Single Blog Title

This is a single blog caption
17
May

wivu wa mapenzi watajwa kuwa chanzo cha vifo;

BIHARAMULO

Viongozi wa Dini wametakiwa kujikita katika kutatua migogoro ya ndoa, ardhi na kulinda maadili ya Watoto ili kuepuka mauaji ya mara kwa mara ikiwa ni sehemu ya kujenga taifa lenye Hekima na kuepuka vitendo viovu

Kauli hiyo imetolewa na aliyekuwa kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Kagera ACP Willium Mwampagare ambaye sasa amehamishiwa Mkoa wa Kaskazin Pemba wakati akizungumza na viongozi wa kada mbalimbali katika Wilaya ya Biharamulo kwenye ukumbi wa Rest House Mei 15 mwaka huu.

Katika kikao hicho maalumu cha kueleza mambo mbalimbali ya Polisi jamii Kamanda Willium mwampagale amesema kuwa Mkoa wa Kagera una vitendo vingi vya mauaji ambapo kuanzia januari mpaka mwezi huu jumla ya watu 65 wamefariki Dunia na sababu kubwa zinazoripotiwa ni wivu wa mapenzi.

Mwampagare ameongeza kuwa vitendo vingine vilivyokithiri ni Wizi wa Mifugo unaosababishwa na kuwa na Mazizi yasiyo salama na kuajiri wachungaji wa mifugo wasiojulikana wanapotokea kwa kigezo cha gharama ndogo Pamoja na kushuka kwa maadili ndani ya jamii na hii ni kutokana na wazazi, walimu na viongozi kushindwa kutimiza wajibu wao kila mmoja kwa nafasi yake.

Aidha ametumia nafasi hiyo kuwataka viongozi wa Dini, mila na serikali ndani ya jamii kujikita kwenye utatuzi wa migogoro ya jamii kikamilifu na kuifikisha kwenye vyombo vya dola hususani polisi ili kuepuka vinyongo vinavyosababisha mauaji au kuficha waharifu.

Nao baadhi ya wananchi na viongozi waliohudhulia semina hiyo ya kuelimishana juu ya Polisi jamii akiwemo Mosoud Geo katibu wa UVCCM Biharamulo salvatory magesa mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo, Alen Rukara Mwenyekiti wa bodaboda na Rashid Omary wameshukuru kutembelewa na Kamanda wa polisi Mkoa kutoa elimu ya Kipolisi kwa jamii na kugusa hoja muhimu zinazogusa wananchi na kwamba ujio huo wa RPC Kagera utaongeza chachu ya mabadiliko ya tabia za mauaji, wizi na upotofu wa maadili.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

You are donating to : FADECO

How much would you like to donate?
$10 $20 $30
Would you like to make regular donations? I would like to make donation(s)
How many times would you like this to recur? (including this payment) *
Name *
Last Name *
Email *
Phone
Address
Additional Note
paypalstripe
Loading...