Single Blog Title

This is a single blog caption
20
May

Wauguzi mkoani kagera wapongezwa kwa kazi nzuri;

Wauguzi Mkoani Kagera wamepongezwa kwa kazi wanayoifanya ya kuhakikisha wanatimiza wajibu wao ikiwemo kuwahudumia wagonjwa kwa haraka ili kuokoa vifo visivyo vya lazima

Akizungumza katika sherehe za maadhimisho ya Wauguzi Duniani ,Mgeni Rasimi Dr Jerad Manase , kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa makao makuu Dodoma,ambapo kimkoa yamefanyika katika Ukumbi wa Wanyama mei 19 mwaka huu

Dr Manase amesema atahakikisha anasimamia vizuri changamoto walizozitaja ikiwemo Upandishaji vyeo kwa wauguzi ambapo pia ametoa hofu kuwa serikali inaendelea kutoa  ajira katika Idara mbalimbali ikiwemo wauguzi

Naye kaimu Muuguzi mkuu Mkoa wa kagera,Neema Kyambo,Amesema wauguzi wanapaswa kuzingatia kanuni  zote za kazi ikiwa ni pamoja na maadili na upendo kwa wagonjwa ambapo pia amewataka kuchukua tahadhari kadri ya kanuni zinavoelekezwa ili kujiweka salama na maambukizi kwani wapo hatarini kupata maambukizi

Awali katika Risala ilisomwa na Katibu wa chama Cha Wauguzi  Mkoa wa kagera(TANNA) Charles Ngalwela amesema licha ya kuwepo kwa mafanikio katika idara ya uuguzi bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo wauguzi kutopandishwa madaraja ,Uhaba wa wauguzi pamoja na   ukosefu wa nyumba za kuishi katika mazingira ya kazi

Kwa upande wao baadhi ya wauguzi wamesema maandisho hayo yamekuwa yakiwasaidia kuwakumbusha wajibu wao ili kusimia misingi Imara katika Kazi pasipo kukiuka maadili pindi wawapo kazini

Sikukuu ya Wauguzi Duniani ni kumbukumbu ya Sherehe za maadhimisho ya Mwanzilishi wa taaluma ya uuguzi Bi Frolence Nightingale ambapo maadhimisho hayo yameambatana na kauli mbiu isemayo OUR NURSES OUR FUTURE-MUUGUZI WETU MUSTAKABALI WETU

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

You are donating to : FADECO

How much would you like to donate?
$10 $20 $30
Would you like to make regular donations? I would like to make donation(s)
How many times would you like this to recur? (including this payment) *
Name *
Last Name *
Email *
Phone
Address
Additional Note
paypalstripe
Loading...