Single Blog Title

This is a single blog caption
12
May

Wajasiriamali waeleza jinsi wanavyo nufaika kupitia michezo ya (Umitashumita);

BIHARAMULO

Baadhi ya wajasiriamaji wadogo wadogo katika mji wa Biharamulo wameeleza wanavyonufaika na fursa za michezo katika uwanja wa CCM Biharamulo wakati wa mashindano ya shule za msingi UMITASHUMITA yanayofanyika kuandaa timu ya kanda ya Biharamulo Mjini kabla ya kupata timu ya jumla kuwakilisha Wilaya kwenda ngazi ya Mkoa.

Wameyasema hayo wakati wakizungumza na mwandishi wa kituo hiki na kuongeza kuwa, zinapotokea fursa za kuwakusanya wanafunzi katika michezo mbalimbali ikiwemo Michezo ya UMITASHUMITA hujitokeza kuuza maandazi, miwa na Barafu ambapo kupitia fursa hiyo wanajipatia kipato.

Elisha Jaston, Jaileth Juma na Pricila Romward ni wajasiriamali ambao wananufaika na michezo hiyo kwa kuuza miwa, pipi, barafu na maandazi kwa wanafunzi na kwamba kupitia mkusanyiko huo hujiingizia kipato kidogo kidogo kwa wanafunzi wanaokuwa wakiendelea na michezo yao.

Aidha wametoa Wito kwa jamii hususani wajasiriamali kutumia fursa hizo za biashara ndogondogo kujiingizia kipato pale kunapokuwepo michezo ya Shule za msingi, Sekondari na michezo mingine kwani kufanya hivyo ni sehemu ya kujinufaisha wao wenyewe.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

You are donating to : FADECO

How much would you like to donate?
$10 $20 $30
Would you like to make regular donations? I would like to make donation(s)
How many times would you like this to recur? (including this payment) *
Name *
Last Name *
Email *
Phone
Address
Additional Note
paypalstripe
Loading...