Single Blog Title

This is a single blog caption
20
May

Waandishi wa habari waaswa kutofungamana na upande wowote katika kazi zao;

KAGERA

WAANDISHI wa habari mkoani Kagera wametakiwa kufanya kazi kwa weledi,kufuata maadili ya uandishi wa habari bila upendeleo na kutoshinikizwa na mtu yoyote ili kuepuka kuandika habari za uongo zitakazohatarisha amani ya nchi.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Erasto Siima katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani yaliyofanyika kimkoa mjini Bukoba, Mei, 20,2023 ambapo kidunia uadhinishwa kila mwaka ya Mei, 3.

Siima amesema kubalance ni wajibu wa mwandishi kufuatilia pande zote mbili, mfano kunapokuwepo malalamiko kutoka pande zote, pale mwandishi anapolazimishwa aseme kinyume na usahihi, jambo ambalo linaweza kumpelekea kuwa matatani kwa maana hiyo mwandishi anapaswa kutimiza majukumu yake kwa weledi alio usomea

Hatahivyo amesema waandishi wa habari wa mkoa wa Kagera wamekuwa kichocheo cha maendeleo ya mkoa huo ndani na nje kutokana na kuandika habari za kuutangaza vyema mkoa huo  huku akiwashauri waendelee kutoa ushirikiano.

Kwa upande wake, Peter Matete ambaye ni mwenyekiti wa chama cha mawakili wa kujitegemea mkoani Kagera (TLS) alifafanua juu ya kauli mbiu ya siku hiyo ambapo amesema kuwa mtu yoyote kama hajasikilizwa anakuwa amenyimwa haki ya msingi ya mwanadamu ambayo anapaswa kuipata tangu anapozaliwa .

Naye mwenyekiti wa KPC Mbeki Mbeki amewashauri waandishi kufanya kazi kwa kufuata misingi mikuu ya waandishi wa habari ambayo ni mustakabali wa haki.

Respicius John ni makamu mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika mkoani humo (KCU 1990) ambae pia ni mdau wa habari amewaomba waandishi wa habari kama wadau muhimu kuendelea kuelimisha wananchi hasa wakati wa kuelekea kwenye msimu wa 2023/2024 katika kutunza ubora wa zao la kahawa ili waweze kupata bei kubwa na kunufaika nalo kwa kujiongezea kipato na Taifa kwa ujumla.

Waandishi wa habari Mkoani Kagera wakiwa kwenye picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Bukoba Erasto Siima.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

You are donating to : FADECO

How much would you like to donate?
$10 $20 $30
Would you like to make regular donations? I would like to make donation(s)
How many times would you like this to recur? (including this payment) *
Name *
Last Name *
Email *
Phone
Address
Additional Note
paypalstripe
Loading...