Single Blog Title

This is a single blog caption
22
May

MAENDELEO YA MRADI WA KUZALISHA NA KUSAMBAZA MICHE YA MIGOMBA KWA NJIA YA TISSUE CULTURE- MKOANI KAGERA 2014-2021

Mwaka 2004, mkoa  wa Kagera ambao ni maarufu kwa uzalishaji wa zao la ndizi, uliingilia na hatimae kushambuliwa na ugonjwa hatari wa munyauko wa migomba au MUNYANJANO au kwa lugha ya kitaalamm, Bacterium Xanthomnas Wilt (BXW). Jitihada mbali mbali za kukabiliana na ugonjwa huu zilianza na kufanyika na wadau mbali mbali.

Njia moja wapo ilikuwa kukata migomba yote iliyokuwa imeshambuliwa, na kuizika. Pengine ilikuwa kutumia njia mbali mbali kama vile kutumia dawa ya kuuwa magugu na njia zingine mbali mbali za kawaidia.

Katika kipindi hicho,WATAFITI katika nchi za Maziwa makuu (Uganda, Rwanda, Kenya na Tanzania) walianza kubuni mbinu mbali mbali za kukabiliana na tatizo la munyauko wa migomba. Ugonjwa huu moja kwa moja uliathiri upatikanaji wa chakula na kuhatarisha ustawishaji wa zao la mgomba. Katika kipindi hiki, kuliibuliwa pia njia ya ki maabara ya TISSUE CULTURE.

FADECO BIOCROPS ambacho ni kitengo cha utafiti na maendeleo ya kilimo chini ya Mkrugenzi wake Joseph Sekiku, baada ya kumaliza mkataba wake na shirika la kimataifa la INIBAP (International Network for the Improvement of Bananas and Plantains alikofanya kazi kwa kipindi cha 2002-2007) walianzisha kitengo cha kuendeleza na kuzalisha migomba isiyokuwa na magonjwa ya TISSUE CULTURE. Shirika la INIBAP kwa sasa linajulikana kama Bioversity International.

Mwaka 2014, FADECO ilianzisha kitaru katika kituo chake cha Kyanyamisa katika kijiji cha Nyakasimbi, na kuanza kuzalisha na kusambaza miche iliyozalishwa kwa njia ya Tissue Culture. Mradi huu umeendelea tangia mwaka 2005 hadi 2021 kwa mafanikio kiasi.

 1. Kuwafundisha wataalam katika uzalishaji na usatawishashaji wa miche ya migomba kwa njia ya Tissue culture.
 2. Awali kundi la wakulima na baadhi ya wataalam walishiriki mafunzo nchini Uganda kupitia ziara maalum katika Maabara ya Kawanda yenye kubobea katika masuala ya Tissue Culture
 3. Vijana 2 walifadhiliwa kushiriki mafunzo katika Maabara ya Kampuni ya BIOCROPS (U) Ltd
 4. Ziara za mafunzo zilifanyika katika maabara mbali mbali za kuzalisha Tissue culture banana za makapmpuni haya:

Agro-genenetic Engineering (Kamapala)

NARO Biotech laboratories

Bio tech laboratory- Jinja (Uganda)

Mwaka 2018, FADECO BIOCROPS tulianza ushirikiano na kampuni ya CROP BIOSCIENCE SOLUTIONS –Arusha, iliyokuja kuwekeza katika mradi mkubwa wa Biotechnology. Na baadae tumeshirikiana na kampuni ya Maua Mazuri kutoka Moshi. Aidha upande wa utafiti, FADECO BIOCROPS tumeshirikiana na wadau wengine akiwemo:

 • Kituo cha utafiti cha Kilimo TARI Mikocheni
 • Kituo cha utafiti cha TARI Kibaha
 • Shirika la MEDA
 • Kituo cha utafiti cha TARI MAruku

Elimu na hamasa ya migomba ya tissue Culture kwa njia ya Radio FADECO:

Awali, pamoja na kitaru cha kuzalisha na kukuza migomba kwa njia ya Tissue Culture, tulianzisha shamba la maonyesho (shamba darasa). Tulihudhuria maonyesho ya kilimo (nane nane katika maeneo mbali mbali kiwilaya lakini pia mkoani).

Kupitia RADIO FADECO tulianzisha kipindi kijulikanacho MKULIMA MBUNIFU na vipindi mbali  mbali na matangazo vimekuwa vikitayarishwa kuongeza elimu na hamasa kwa wakulima namna ya kulima na kustawisha zao la migomba.

Tathmini fupi:

Katika kipindi cha 2014-2021-FADECO BIOCROPS tumezalisha na kusambaza takribani miche ya migomba 45,000 katika maeneo mbali mbali wilayani Karagwe, Missenyi, Bukoba Vijijini, Kyerwa na Biharamulo.

Tulikutana na changamoto nyingi kama inavyokuwa kwa tekinolojia mpya:

 • Wakulima pamoja na maafisa ugani mkoani Kagera awali hawakuelewa kuwa migomba inaweza kuzalisha kwa njia ya maabara (tissue culture)
 • Uzalishaji wa migomba na gharama za uendeshaji ulilazimu mche wa mgomba kuuzwa kwa shs 3,000/- bei iliyoonekana juu ya uwezo wa wakulima wengi
 • Miche kukaa katika kitaru kwa muda mrefu
 • Mwaka 2019, wakulima na baadhi ya miradi iliyokuwa imekubali kushirikiana nasi, waliamua kuachana na zoezi baada ya mlipuko wa ugonjwa wa COVID 19, na hivyo kupelekea kuzorota kwa usambazaji wa migomba.

Mwaka 2023:

Kwa mara ya kwanza, utumiaji wa migomba iliyozalishwa kwa njia ya tissue culture, limejadiliwa Bungeni kufuatia hotuba ya bajeti aliyowasilisha Waziri wa Kilimo.

IMPACT YA MRADI NA MCHANGO WA FADECO BIOCROPS katika usambazaji wa migomba iliyozalishwa kwa njia ya Tissue culture:

Wakulima wanasema, migomba yao waliyoipata kutoka kwenye mradi, haijawahi kushambuliwa na munyauko

 • Wengi (wote) wameisha nufaika na chakula na mauzo kutokana na migomba hiyo
 • Wakulima wameweza kupanua mashamba yao ya migomba hiyo
 • Wengi wameweza kuwasambazia wakulima jirani, miche ya migomba kutokana na migomba walioipata kutoka kwenye mradi
 • Migomba ya Tissue Cultre iliweza kustahimili na kufanya vizuri pale ambapo migomba mingine ya asili ilishindikana

MIPANGO YA BADAE:

FADECO BIOCROPS tuna uzoefu na tekinolojia ya uzalishaji na ustawishaji wa migomba kwa njia ya Tissue culture. Ikiwa kunakuwpo na hitaji, miundo mbinu na ujuzi tunao.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

You are donating to : FADECO

How much would you like to donate?
$10 $20 $30
Would you like to make regular donations? I would like to make donation(s)
How many times would you like this to recur? (including this payment) *
Name *
Last Name *
Email *
Phone
Address
Additional Note
paypalstripe
Loading...