Single Blog Title

This is a single blog caption
11
May

Jumla ya shilingi milioni 53,066,000 zatumika katika ukarabati wa miundombinu ya masoko wilaya ya Biharamulo;

BIHARAMULO

Na Sadoth Leo Trazias

Kata ya Biharamulo mjini Wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera imepokea shilingi milioni 53,066,000 kwa ajili ya ujenzio na ukarabati wa miundombinu ya masoko ya kasusura na soko jipya kutokana na fedha za mfuko wa jimbo na mapato ya ndani ya Halmashauri.

Akizungumza na Fadeco radio Diwani wa Kata ya Biharamulo mjini David mwenenkundwa amesema kuwa fedha hizo zinakwenda kutatua changamoto ya uhaba wa matundu ya vyoo soko la kasusura na ukarabati wa vyumba 10 vya Bucha kwenye masoko yote mawili ikiwa ni Pamoja na kukarabati vibanda vya Biashara ili kuongeza ukusanyaji wa mapato ya halmashauri.

Amesema kuwa miradi hiyo mahususi itasaidia kuongeza ujira kwa vijana wanaofanya kazi ya vibarua kwa kujiingizia kipato na ametoa wito kwa wananchi wa Biharamulo kutunza miradi hiyo vizuri ili iwanufaishe watumiaji wake.

Aidha mwenenkundwa ameeleza miradi mingine inayotarajiwa kujengwa kata hiyo kuwa ni ujenzi wa Barabara kilometa mbili kwa kiwango cha lami kuanzia bajeti ya 2023/24, ujenzi wa chuo cha VETA Eneo la Kanywamaizi mradi ambao ameutaja kuwa utaongeza tija ya mzunguko wa fedha kuanzia kwa mama na babalishe, waendesha pikipiki, vibarua na wanabiharamulo watakaowekeza kujenga nyumba za wapangaji kwa ajili ya malazi kwani chuo kitadahili wanachuo kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.

Hata hivyo ameipongeza serikali kuu, Halmashauri ya Biharamulo kupitia mapato ya ndani na mbunge wa jimbo la Biharamulo magharibi mhandisi Ezra Chiwelesa kupitia mfuko wa jimbo kuwezesha upatikanaji wa fedha hizo za ukarabati ambazo zinakwenda kusaidia wajasiriamali kufanya kazi kwenye mazingira salama.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

You are donating to : FADECO

How much would you like to donate?
$10 $20 $30
Would you like to make regular donations? I would like to make donation(s)
How many times would you like this to recur? (including this payment) *
Name *
Last Name *
Email *
Phone
Address
Additional Note
paypalstripe
Loading...