Habari za Michezo

MULEBA:

Kutoka katika meza ya Afisa Utamaduni na Michezo, wilayaya Muleba Bw. Denis Joseph, anapenda kuwajulisha viongozi na wanachama wa vyama vya Michezo vyote wilayani Muleba,

  1. kutayarisha na kupeleka mpango kazi wa mwaka 2024 na taarifa ya  ale yaliofanyika mwaka 2023 kwa kila Chama tuyapte Kabla ya  tarehe  1/4/2024 saa Sita kamili niombe tulikamilishe kwa uharaka wake .
  2. vyama vyote vya michezo vikae vikao na tunaomba muhtasari wa vikao hivyo nakala lengo kuinua vyama vyetu na kuondoa migogoro ndani ya wanachama kaeni na wanachama wenu .
  3. Kaeni na wadau wenu kwa kuwafuata kila tarafa ili kuwa na kitu cha pamoja.
  4. Panga na ratibu mafunzo ya kila Chama ili kuongeza utaalamu katika vyama na wanachama wenu .

Vyama hivyo ni hivi vifuatavyo.

1.CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU MDFA

2.CHAMA CHA MPIRA WANAWAKE MDWAF.

3.CHAMA CHA WAAMUZI W

4.CHAMA CHA MICHEZO YA JADI W

5.CHAMA CHA SKAUTI W

6.CHAMA CHA MCHEZO WA MPIRA WA MIKONO MDHA

7.CHAMA CHA MCHEZO WA MPIRA WA WAVU MDVA.

8.CHAMA CHA MCHEZO WA RIADHA.

Wakati huo huo, Afisa utamaduni na michezo wilaya ya Muleba anapenda kuwatagazia kuwa mafunzo ya walezi wa skauti shule za msingi yanaendelea tarafa zetu tano yakiendeshwa na mkufunzi toka Taifa lengo ikiwa ni kuendeleza uzalendo wa taifa letu.

Pia anawataarifu kuwa, kuna ujio wa timu ya Umisseta sekondari ya mkoa wa Geita kwa michezo mbalimbali ikiwemo netball na soka wapo katoke chuo chuo cha ualimu kwa wiki kadhaa lengo ni kuzipa timu zetu za wilaya mbinu mbalimbali kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya umisseta na umitashumita mkoa na taifa na mkufufunzi wa netball wa kitaifa anaetoka geita mpira unatembelea michezo mbalimbali.

Na siku ya jumanne wiki iliyopita, Uongozi wa Muleba Youth Sports Centre waliweza kusaini mkataba wa ushirikia Kati ya Azam Fc & Muleba Youth Sports Centre na mkataba huu umelenga zaidi kiwasaidia vijana wenye vipaji na kuwaunganisha pamoja kwenye soko la mpira wa miguu.

You are donating to : FADECO

How much would you like to donate?
$10 $20 $30
Would you like to make regular donations? I would like to make donation(s)
How many times would you like this to recur? (including this payment) *
Name *
Last Name *
Email *
Phone
Address
Additional Note
paypalstripe
Loading...