Single Blog Title

This is a single blog caption
11
May

Bilioni 15.9 zapeleka neema mgodi wa STAMIGOLD Biharamulo;

BIHARAMULO

Bilioni 15.9 zapeleka umeme mgodi wa STAMIGOLD Biharamulo.
Sirika la umeme nchini (TANESCO) mkoa wa Kagera limetumia zaidi ya shilingi Bilioni 15.9 kujenga na kukamilisha mradi mkubwa wa njia ya kusafirisha umeme wa gridi ya Taifa wa kilovoti 33 ulioanza kutumika kwenye mgodi wa dhahabu wa STAMIGOLD Biharamulo mkoani Kagera na hivyo kupunguza gharama kubwa za ununuzi wa mafuta ya jenereta zilizokuwa zinatumika awali kuendesha shughuli za mgodi huo.
Kwa mujibu wa Meneja wa TANESCO mkowa Kagera, Mhandisi Godlove Mathayo, amesema wameunganisha umeme kwenye mgodi huo wa STAMIGOLID Biharamulo ikiwa ni jitihada za shirika kupeleka huduma hiyo kwenye migodi ili kuongeza tija ya uzalishaji na kuleta manufaa kwa uchumi wa Taifa kupitia sekta ya madini.
Naye meneja wa mradi huo, Mhandisi Dismas Masawe, amesemq ujenzi wa mradi wa njia ya kupeleka umeme wa gridi ya Taifa kwenye mgodi wa STAMIGOLD Biharamulo ulianza mwezi Augost mwaka 2020 na baada ya kukamilika kwake sasa wanaanza jitihada za kuunganisha umeme kwenye mgodi wa dhahabu wa Geita mkoani Geita yaani GGML.
Mkandarasi kutoka kampuni ya ITDICO iliyotekeleza mradi huo, Mhandisi Mustapha Himba, amesema ujenzi wa njia ya umeme umefanyika katika eneo la umbali wa kilometa 105 kutoka kituo cha kupokea umeme cha Mpomvu mkoani Geita ukihusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme pamoja na kituo cha kupokea na kupoza umeme cha STAMIGOLD Biharamulo chenye transfoma mbili.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Biharamulo, Kamishna msaidizi wa polis (ACP) Advera Bulimba, ametoa wito kwa wawekezaji wengine kuwekeza wilayani Biharamulo kwani kuna mazingira rafiki ikiwemo uwepo wa umeme wa uhakika.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

You are donating to : FADECO

How much would you like to donate?
$10 $20 $30
Would you like to make regular donations? I would like to make donation(s)
How many times would you like this to recur? (including this payment) *
Name *
Last Name *
Email *
Phone
Address
Additional Note
paypalstripe
Loading...