Single Blog Title

This is a single blog caption
19
May

Zaidi ya milion, 500 kutumika kuboresha miundombinu ya shule ya msingi Bunazi;

KAGERA

Na Shahidu  Kyagulani

Zaidi ya shilingi milioni 500 zimetengwa kwa ajiri ya ujenzi wa shule mpya ya  Bunazi itakayo jengwa eneo la pembezoni mwa shule kongwe

Hayo yamebainishwa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya  ya missenyi Waziri Komba alipokuwa akizungumza na kituo hiki na kusema kuwa fedha hizo zimetoka serikali kuu kupitia mradi wa Kusukuma miundo mbinu ya Elimu, (boost)kwa ajiri ya kuimalisha sekta ya elimu inchini

Waziri komba amesema fedha hizo zitatumika katika ujenzi na ukarabati wa shule ya Bunazi ikiwemo kujenga vyumba 2 vya madarasa ya awali na matundu 6 ya vyoo  pamoja na vyumba 14 vya madarasa  kwa Elimu ya msingi, matundu 18 ya vyoo  na jengo la Utawala na Vichomea taka 2.

Hatahivyo ameipongeza serikali ya Rais Samia Suluhu Hassani, namna anavyo imejipanga katika kushughurikia changamoto katika secta ya elimu na kwamba wananchi wanapaswa kuhakikisha wanatunza miundombinu zote zitakazojegwa kwenye mradi huo.

Nae Diwani wa kata hiyo Mh yusuphu mzumbe amewataka wananchi kuendelea kujitolea kwenye shughuli za maendeleo kwa kuunga mkono jitihada za serikali huku akiwataka wananchi wa Kijiji cha nyabihanga kuwa na ushirikiano katika jamii

Abdulhamidu Abdalla ni mwenyekiti wa kamati ya shule ya bunazi ambapo ameipongeza serikali kwa kuwapatia fedha hizo na kwamba itasaidia kuondoa changamoto ikiwemo wingi wa watoto wanao somea shule hiyo kongwe kukosa madarasa

Aidha nae mkuu wa shule hiyo Mukama Waso,amewashukuru wazazi na walezi kwa kuamua kujitolea kuandaa usafi kwenye eneo litakalo tumika kujenga shule hiyo, na kuongeza kua kukamilika kwa ujenzi wa shule hiyo kutasaidia kuongeza ufauru wa wanafunzi kwani watakua na walimu wakutosha,sambamba na uhuru wa kukaa kwa wanafunzi darasani.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

You are donating to : FADECO

How much would you like to donate?
$10 $20 $30
Would you like to make regular donations? I would like to make donation(s)
How many times would you like this to recur? (including this payment) *
Name *
Last Name *
Email *
Phone
Address
Additional Note
paypalstripe
Loading...