Single Blog Title

This is a single blog caption
09
May

Baadhi ya taka zinazotupwa jalalani zimetajwa kuwa dili;

BIHARAMULO

KATIKA kuunga juhudi za usafi wa mazingira mjini Biharamulo Mwalimu mstaafu na mkurugenzi wa kituo cha kulea Watoto wadogo Topstar Rukaragata,   Felix Bilego Amebuni mbinu mpya ya  kukusanya baadhi ya taka na kuzichakata kuwa katika hali ya bidhaa nyingine.

Akizungumza na kituo hiki akiwa kwenye eneo la kuchakata  baadhi ya taka ngumu  amesema lengo na madhumuni   ni kusafisha mazingira Pamoja na kuwasaidia vijana kutambua na kufahamu fulsa zinazo wazunguka.

Aidha amesema taka ambazo zimekuwa zikitumika ni mabokisi yaliyo isha matumizi  ambayo yanatumika kutengeneza sanamu za  mapambo ya ndani,nasamani chakavu hutumika kutengeneza zana za kufundishia ambayo itakuwa mwarobaini wakutatua uhaba wa zana zakufundishia kwa waalimu na kwamba walimu  wanatakiwa kutembelea ofisi zake ili kuweza kupata  zana za kufundishia.

Milton Philimoni ni mmoja wa vijana ambao wanafanya kazi ya kutengeneza zana hizo Pamoja na kuchonga sanamu ameeleza namna ubunifu huo unavyo mpatia kipato nakukidhi mahitaji yake hivyo amewataka vijana wenzake wilayani biharamulo kujitokeza kujifunza Sanaa na hivyo kuwasaidia kupambana na changamoto ya ajira.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

You are donating to : FADECO

How much would you like to donate?
$10 $20 $30
Would you like to make regular donations? I would like to make donation(s)
How many times would you like this to recur? (including this payment) *
Name *
Last Name *
Email *
Phone
Address
Additional Note
paypalstripe
Loading...