Single Blog Title

This is a single blog caption
11
May

Ahukumiwa jera miaka 30 kwa ubakaji;

BIHARAMULO

Na Sadoth Leo Trazias

Mahakama ya Wilaya Biharamulo Mkoani Kagera Imemhukumu Kwenda jera miaka 30 Deogratius Selestine (49) kwa kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 13 katika kijiji cha Nyakahura, Kata ya Nyakahura Wilayani humo.

Mbele ya mahakama hiyo mwendesha mashtaka wa polisi Edith Tuka ameieleza mahakama kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo la ubakaji kwa kumshawishi mtoto huyo kuingia kwenye nyumba yake julai 30 mwaka 2022 majira ya saa 12 jioni na kumtendea unyama huo.

Imedaiwa mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa alifikishwa mahakamani Agosti 04 mwaka 2022 kwa kesi ya jinai namba 101 ya mwaka 2022 na kusomewa shitaka lake ambapo ameiomba mahakama kumchukulia hatua kali mtuhumiwa ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.

Imeelezwa kuwa Mtuhumiwa alipoombwa kujitetea kwa kosa alilolitenda ameendelea kujitetea kuwa hakutenda kosa hilo.

Hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama ya Wilaya ya Biharamulo Subira Mashambo ameiambia mahakama kuwa baada ya kusikiliza Ushahidi wa pande zote mbili mahakama imelidhishwa na Ushahidi wa upande wa mashtaka hivyo mahakama inamhukumu Deogratius Selestine Kwenda jera miaka 30 kwa kosa la ubakaji wa mtoto mwenye umri wa miaka 13 ili iwe fundisho kwa wengine.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

You are donating to : FADECO

How much would you like to donate?
$10 $20 $30
Would you like to make regular donations? I would like to make donation(s)
How many times would you like this to recur? (including this payment) *
Name *
Last Name *
Email *
Phone
Address
Additional Note
paypalstripe
Loading...